TANGAZO


Tuesday, May 13, 2014

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana akagua maendeleo ya Wilaya ya Uyui, Maabara za Shule za Sekondari za Kata, wilayani humo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma, Jimbo Tabora, wilayani Uyui, ambapo alizungumzia jinsi serikali  ilivyoazimia kuboresha sekta ya maji, umeme na elimu na barabara vijijini. Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma ambapo waliwafananisha wapinzania na fisi aliyejifanya ana pembe kwenye mkutano wa wanyama wenye pembe na baadaye kuumbuka baada pembe zake alizozinatisha kwa nta kung'oka baada ya kuyeyushwa na jua kali.Kinana akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, ambapo alikagua ujenzi wa nyumba 8 za watumishi ,  Hospitali ya Wilaya, Jengo la Halmashauri ya wilaya hiyo, Kituo cha Polisi. Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa (kushoto) akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga wakati Kinana alipotembelea Makao Makuu ya wilaya hiyo eneo la Isikizya.Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakimsikiliza Kinana alipowatembelea leo.Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Uyui, Steven Nyanda (kulia) kuhusu ujenzi wa nyumba za watumishi wa wilaya hiyo.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Uyui, Mussa Ntimizi.Moja ya nyumba za watumishi wa wilaya ya Uyui zilizojengwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.Kinana akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Uyui eneo la Isikizya.Kinana aakikagua ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya Uyui.Kinana akielekea kukagua chanzo cha maji katika eneo la Isikizya.Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa akielezea jinsi alivyofanya jitihada za kuuendeleza makao makao makuu ya wilaya ya Uyui.Kinana na Nape wakikagua ujenzi wa nyumba 50 za watumishi.Kinana, Nape wakipanda miti katika eneo la Shule ya Sekondari ya Ilolangulu wilayani Uyui.Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga akitoa taarifa ya utekelezaji wa  Ilani ya CCM katika wilaya hiyo.Kinana akihutubia katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Uyui ambapo alisomewa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.Mwalimu wa somo la kemia wa Shule ya Sekondaro Ndono, wilayani Uyui, Mahubira Chandarawa akimuonesha Kinana jinsi ya kutumia vifaa vya maabara alipokagua maabara ya shule hiyo ya Kata.Nape  9mbele0 akikagua jengo la maabara la Shule ya Sekondari ya Ndono, wilayani Uyui.Kinana akikagua jengo la Zahanati ya Kata ya Ufuluma, Tabora Kaskazini, wilayani Uyui.Kinana akiwasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma, wakati wa ziara yake wilayani Uyui.Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa Tabora, Mwanne Nchemba, akihtubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma.Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Ufuluma ambapo azingumzia matatizo yanayowakabili wakuliama wa zao la tumbaku.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, akizungumza katika mkutano huo wa hadhara na kuelezea jitihada zinazofanywa kuboresha sekta ya afya, elimu, maji na barabara wilayani humo.Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini, Shaffin Sumar na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Lucy Mayenga wakisikiliza kwa makini wakati Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano huo.Kinana akiwa na Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Uyui, ambaye alimtaka kuelezea mipango ya ujenzi wa visima saba katika Kata ya Ufuluma.Baadhi ya wana CCM wakila kiapo cha utii cha chama hicho  katika mkutano huo.Baadhi ya walimu wa Wilaya za Uyui na Tabora Mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, alipokuwa akizungumza nao kuhusu matatizo mbalimbali yanayowakabili na jinsi ya kuyasuluhisha.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akizungumza na waalimu wa shule katika Wilaya za Uyui na Tabora Mjini, jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo kukatwa sehemu ya mishahara yao, kunyimwa fedha za zikizo,  ukiritimba wa kupandishwa vyeo na mengineyo. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment