Takriban watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na wapiganaji wa Ahlu Sunnah wal Jama'a kukabiliana na wapiganaji wanaounga mkono utawala wa muda wa eneo la Juba eneo la,Buulo Haawo, Kusini Magharibi mwa Somalia.
Wapiganaji watiifu kwa utawala wa Jubba wamedhibiti sehemu kubwa ya mji .
Duru za serikali zinasema kuwa waziri mkuu Abdiweli Shaykh Ahmad anaunga mkono serikali ya Jubba na amekuwa akifanya mazungumzo na Ethiopia kuhusu swala hilo.
Gavana wa jimbo la Gedo, Muhammad Abdi Kalil, aliambia redio Shabeelle kuwa wapiganaji wanaounga mkono utawala wa Jubba walishambulia mji huo baada ya kupokea silaha kutoka mjini Doolow town.
Afisa mmoja wa kundi la Ahlu Sunnah Muhammad Husayn Al-qadi, pia aliambia redio Shabeelle kuwa shambulio dhidi ya Buulo Xaawo lilipangwa katika ofisi ya waziri mkuu.
No comments:
Post a Comment