TANGAZO


Monday, May 19, 2014

Rais Kikwete aongoza kuuaga mwili wa Mwakapugi jijini Dar

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini marehemu Arthur Mwakapugi, huko nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam jana. Mwakapugi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 64, alilitumikia Taifa kwa miaka 30 mfululizo katika nafasi mbalimbali. Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake, Ilundo Wilaya ya Tukuyu, Mbeya. (Picha zote na Freddy Maro).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini marehemu Arthur Mwakapugi, nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam jana. 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini marehemu Arthur Mwakapugi, nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam jana. Mwakapugi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 64 alilitumikia Taifa kwa miaka 30 mfululizo katika nafasi mbalimbali. Mwili wa marehemu baadaye ulisafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwake, Ilundo wilayani ya Tukuyu, Mbeya.

No comments:

Post a Comment