Mkurugenzi
wa Fadhila FM Redio, Edwin Mpokasye akiwakaribisha washiriki katika
ufunguzi wa warsha ya Maadili na kuandika Habari za Jinsia na Migogoro
kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani
Mtwara.
Mkurugenzi
wa Fadhila FM Redio, Edwin Mpokasye akikabidhi risala aliyoitoa kwa
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Farida Mgomi wakati wa hafla fupi ya ufunguzi
wa warsha hiyo.
Mshauri
na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa
ufafanuzi kuhusu madhumuni ya warsha hiyo inayoendeshwa chini mradi wa
Democratic Empowerment Project (DEP) unaofadhiliwa na Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kutekelezwa na UNESCO. Kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi. Farida Mgomi.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi. Farida Mgomi, akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Maadili na kuandika Habari za Jinsia na Migogoro kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
Mshiriki wa warsha Hassan Hassan kutoka Kituo cha Redio Micheweni FM, Pemba, akiwasilisha kazi ya kikundi kazi.
Pichani
juu na chini ni washirki kutoka Redio Jamii za Micheweni, Mtegani,
Zenji, Pangani na Fadhila waliohudhuria warsha ya siku 10 iliyofanyika
kwenye kituo cha Redio Fadhila FM Masasi.
Mshauri
na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu
akiendesha mafunzo ya Jinsia kwa washiriki wa warsha ya Kuandika Habari
za Migogoro Kimaadili kwa waandishi wa habari wa Redio za Jamii
iliyofanyika Masasi mkoani Mtwara.
Mshiriki
kutoka Pangani FM Redio, Abdilhali Shukurani (kushoto-mwenye shati
nyeupe), akichangia mada ya Jinsia na Uchaguzi wakati Mkufunzi wa
mafunzo hayo Bi. Rose Haji Mwalimu akimsikiliza kwa makini.
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Bi Farida Mgomi (wa pili kulia).
No comments:
Post a Comment