Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu waziri Mawasiliano Sayansi na Technolojia na mbunge wa Bumbuli January Makamba wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Bumbuli Shughuli hiyo imefanyika katika Hotel ya Golden Tulip leo (Ijumaa) Tarehe.16.05.2014. (Picha zote na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wimbo wa wanabumbuli mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip kwa ajili ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kilutheri la Bumbuli, Kushoto ni askofu mkuu wa KKKT Dr.Gerhas Malasusa, Watatu Kulia ni Dkt.Steven Munga wa Lushoto na kulia ni mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mh. January Makamba Katika harambee hiyo, zaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilipatikana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watu walioshiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la KKKT Bumbuli jana iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam jana jioni.Walioketi mbele Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania Askofu Gerhaz Malasusa,Askofu wa Lushoto Steven Munga (wanne kushoto) na watano kushoto ni Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba.Zaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilikusanywa katika harambee hiyo ikiwa ni ahadi,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu.
No comments:
Post a Comment