Wizara ya afya nchini Libya
imesema zaidi ya watu 40 wameuwawa mjini Benghazi siku Ijumaa katika
mashambulizi anga na nchi kavu yaliyoongozwa na kanali wa zamani wa
jeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislam.
Vurugu hizo zilizofanyika zinaelezwa kuwa
zilikuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu mapinduzi ya yaliyomuondoa
madarakani Kanal Muamar Gadafi mwaka 2011.Taarifa kutoka mjini Benhgazi zinasema hivi sasa utulivu umerejea kwenye mji huo kama ilivyokuwa awali.
Mtu aliyeogoza mashambulizi hayo, Khalifa Haftar amesema ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa watu wote aliowaita magaidi nje ya mji wa Benghazi.
Serikali kuu imelaani matumizi hayo ya nguvu na kuuita hatua hiyo kama jaribio la mapinduzi lililoshindwa.
No comments:
Post a Comment