Mtu anayetarajiwa kushika
wadhifa wa Waziri Mkuu nchini India Narendra Modi amepongezwa na umati
mkubwa wa wafuasi wake mjini Delhi baada ya chama chake cha BJP kuibuka
mshindi katika uchaguzi mkuu nchini humo.
Bwana Modi ambaye amepanda kutoka kuwa muuza
chai hadi kuwa kiongozi wa watu billioni moja amekutana na viongozi wa
juu wa chama chake cha BJP katika makao makuu ya chama hicho baada
msafara wa maandamano ya kumpongeza kutoka uwanja wa ndege.Mapema hii leo, Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Manmohan Singh aliwasilisha barua yake ya kujizulu kwa rais Pranab Mukherjee.
Katika hotuba yake ya mwisho kwa njia ya televisheni Bwana Singh amesema India imekuwa nchi imara zaidi kuliko ilivyokuwa mionogo kadhaa iliyopita wakati alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu.
No comments:
Post a Comment