Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE)
Mkoa wa Dar-es-salaam, Bw. Hassan Kaumo akiongea na wafanyakazi wa
Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la
Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 30, 2014).
Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Fanuel Mbonde. (Picha zote na
Martha Komba - Wizara ya Katiba na Sheria)
Baadhi
ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria katika mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi la Wizara hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika mkutano wa Baraza hilo la Wafanyakazi la Wizara, Dar es Salaam leo.
Na Martha Komba, Dar es Salaam
WATUMISHI wa Wizara ya Katiba na Sheria wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Bw. Fanuel Mbonde amesema hayo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi
la Wizara hiyo uliofanyika leo (Jumatano April 30, 2014) jijini
Dar-es-salaam.
“Uwajibikaji ni suala muhimu sana katika
utumishi wa umma,” alisema katika mkutano huo wa siku moja uliofanyika
katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar-es-salaam.
Aidha, Katibu Mkuu huyo aliwasihi
watumishi wote wa Wizara yake kuungana na wafanyakazi wote nchini na
duniani kushiriki katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi zinazofanyika
kesho (Alhamisi, Mei 1, 2014).
Awali akiongea katika mkutano huo,
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Mkoa wa
Dar-es-salaam Bw. Hassan Kaumo aliwataka watumishi wa Wizara hiyo
kutimiza wajibu wao katika sehemu zao za kazi.
“Tunapodai maslahi ni lazima pia
tusisitize kutimiza wajibu. Wafikishieni salamu hizi wafanyakazi wote,
wachape kazi ili watupe viongozi nguvu ya kudai maslahi bora,” alisema
Kaumo katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi na wawakilishi wa
wafanyakazi kutoka Idara na Vitengo vyote vya Wizara hiyo.
Mkutano huo, pamoja na mambo mengine,
ulijadili maslahi ya watumishi na kupitia na kuridhia Taarifa ya Mpango
wa Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha 2014/2015.
No comments:
Post a Comment