*Wizara yamaliza kazi ya kuipitia Katiba ya Simba
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania Ndg. Leornad
Thadeo, akifafanua na kutowa kwa waandishi wa kuhusiana na Rasiomu ya
Katiba ya Timu ya mpira wa miguu ya Simba baada waandishi kutaka
ufafanuzi juu ya Katiba ya Uchaguzi Klabu ya Simba.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Tanzania Ndg. Leornad Thadeo,akiwaonesha waandishi habari Rasimu ya Katiba ya Timu ya Simba, baada ya wandishi kutaka ya Uchaguzi Mkuu wa Timu ya Simba, unaotaraji kufanyika wakati wowote.(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
Na Genofeva Matemu –
Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)
30TH
April, 2014
SERIKALI kupitia
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya
Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya Club ya
Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw.
Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali za
waandishi leo jijini Dar es Salaam.
Akijibu moja ya hoja
iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika upatikanaji wa Katiba ya Club
ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji wa Katiba umemelizika na kuonekana
kuwa na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze
kuidhinisha katiba hiyo.
“Mchakato wa upitiaji
wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini kumekuwepo na mapungufu
machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha Katiba hiyo”
amesema Bw. Thadeo.
Akifafanua zaidi Bw.
Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande wa kisheria ambapo
mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana tofauti na Katiba
ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya marekebisho hayo mapema na
kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya kuidhinishwa.
No comments:
Post a Comment