TANGAZO


Saturday, April 12, 2014

Mwenyekiti wa Bungeni Maalum la Katiba alazimika kuaghirisha kikao cha kuwasilisha Ripoti za Kamati

*Ni kutokana na TBC kukata matangazo ya kurusha moja kwa moja uwasilishwaji wa Ripoti
*Ilikuwa ni katika kuwasilishwa kwa maoni ya wachache
*Asema lazima haki itendeke
*Asema hataki kuonekana anapendelea

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa mwongozo kwa wajumbe wa Bunge hilo leo mjini Dodoma juu ya kuzingatia yaliyoandikwa katika taarifa za Kamati mbalimbali za Bunge hilo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.bogspot.com)
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa maelekezo kwa wajumbe wa bunge hilo, leo mjini Dodoma, kuhusu kuzingatia yaliyoandikwa katika taarifa za Kamati mbalimbali wakati wa uwasilishwaji wa taarifa Kamati za Bunge hilo.
Mjumbe kutoka Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba Dkt. Hamis Kigwangalla akiwasilisha 
maoni ya Kamati hiyo kwenye kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Mjumbe kutoka Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba Dkt. Hamis Kigwangalla akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo, kwa wajumbe waliwengi kwenye kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Mjumbe kutoka Kamati namba tatu (3) ya Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Peter Msigwa akiwasilisha maoni ya wachache kwenye kamati hiyo, katika kikao cha Bunge leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia uwasilishaji wa ripoti za Kamati mbalimbali, ndani Bunge leo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto), wakibadlishana mawazo na Mjumbe kutoka Kamati namba tatu (3) ya Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Peter Msigwa leo mjini Dodoma.
Mjumbe kutoka Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya wachache ya kamati hiyo, kwenye kikao cha bunge leo mjini Dodoma.
Mjumbe kutoka Kamati namba nne (4) ya Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu akinukuu moja ya vitabu vya waandishi mahiri katika masuala ya Muungano, wakati alipokuwa akiwasilisha maoni ya wachache ya kamati hiyo, kwenye kikao cha bunge leo, mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta, akimtka mmoja wa wajumbe wa bunge hilo, kutoa hoja kuhusu kuaghirishwa kwa kikao cha bunge hilo, kutokana na kukatika matangazo ya moja kwa moja ya TBC, yaliyokuwa yakirushwa na kituo hicho wakati wa uwasilishwaji wa maoni ya wachache na mjumbe Tundu Lissu wa kamati namba 4, leo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (katikati),akimpongeza mjumbe mwenzake, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu (kushoto), nje ya ukumbi wa Bunge, kutokana na alivyokuwa akiwasilisha hoja za wachache katika kamati yao, namba 4 ya bunge hilo, kwenye kikao cha uwasilishaji ripoti wa kamati zote 12 ndani ya ukumbi Bunge, mjini Dodoma leo. Kulia ni mjumbe mwenzao, Mchungaji Peter Msigwa.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiondoka eneo la Bunge leo, mjini Dodoma baada ya kikao kuagharishwa.

No comments:

Post a Comment