*Akutana na wavuvi wadogo wadogo wa Ziwa Tanganyika
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya nyumba ya Makumbusho ya Dr. Livingstone, iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma leo.
Katibu Mkuu wa CCM (wa tatu kulia), Kinana pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama hicho, Mkoa na Wilaya wakipata maelezo mafupi kuhusiana na historia ya mnara huo, ambao Dr. Livingstone na Henry M. Stanley walikutana kwa mara ya kwanza katika mji wa Kihistoria wa Ujiji, mkoani Kigoma katika suala zima la kusambaza dini na kupambana na biashara ya Utumwa.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na mama Mawazo Rashid Mawala, mkazi wa Ujiji Kigoma. Katibu Mkuu alikuwa akitembea kwenye njia (route) iliyotumika na Watumwa ambapo kuna miembe yenye umri zaidi ya miaka 150, miembe kama hii, inapatikana sehemu ya Tabora na Bagamoyo.
Sehemu ya njia (route), kama ionekanavyo pichani, ndani mji wa kihistoria Ujiji, mkoani Kigoma, iliyotumika kusafirishia Watumwa kwenda sehemu mbalimbali, katika njia hiyo, kuna miembe inayoelezwa ina umri zaidi ya miaka 150 tangu kupandwa kwake na inaelezwa inapatikana sehemu za Tabara na Bagamoyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Masoud Mwinyi Chande kwenye mnara wa kumbukumbu ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji, wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Inaelezwa kuwa Nyumba hiyo Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadiri na Bibi Titi Mohamed. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, Katibu wa NEC, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye, pamoja na Mwenyekiti wa CCM-Kigoma Amani Kabouru.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akielekezwa sehemu ya chumba na mlango ndani ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Nyumba hiyo inasemekana Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadiri na Bibi Titi Mohamed.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa, wakiwasilia kwenye Nyumba ya Makumbusho ya Dr. Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma na kujionea mambo mbalimbali ya kihistoria yaliyomo ndani ya jengo hilo.
Mmoja wa wakazi wa eneo la Kibiri,ambalo liko ufukweni kabisa mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma, akibandika mabango yake yenye ujumbe wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahamn Kinana, alipokwenda kutembelea eneo hilo na kusikiliza kero mbalimbali za wavuvi wadogo wadogo.
Baadhi akina Mama ambao ni wafanyabiashara wa samaki na dagaa pamoja na uvuvi, wakiwa wamekusanyika wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kwa ajili ya kuwazisilisha kero zao, mbalimbali ikiwemo tozo za kodi na ushuru mkubwa, ikilinganishwa na kipato chao.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisoma moja ya bango lenye ujumbe wa kulalamikia kodi kubwa wanazotozwa wavuvi wadogo wadogo wa Kibirizi, Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibirizi, mkoani Kigoma ambao wanakilio cha kutozwa kodi kubwa, kuvamiwa na majambazi wakati wa shughuli zao za uvuvi.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Ofisi mpya ya CCM, Kata ya Kibirizi.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza kwenye kikao cha Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM, katika ukumbi wa Kibo Peak Club, Wilaya ya Kigoma mjini, mkoani humo, ambapo Kinana alizungumza mambo mbalimbali ya kutekeleza na kuhimiza Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010, pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii.
Pichani katikati ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba, akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kushoto), wakati wakielekea kutazama nyumba ya Makumbusho ya Dr. Livingstone, iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma. Kulia ni a Katibu wa NEC, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye. (Picha zote kwa hisani ya Richard Mwaikenda)
No comments:
Post a Comment