TANGAZO


Monday, April 14, 2014

Kikao cha Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo

*Wasira asema Serikali itawasilisha Hati ya Makubaliano ya Muungano siku mbili zijazo
*Ni baada ya Mnyika kutaka mjadala usimame hadi itakapowasilishwa hati hiyo

Mjumbe wa Kamati namba 4 ya Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu, akizungumza wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa Ripoti ya wachache kwenye kamati hiyo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mjumbe wa Kamati namba 4 ya Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu, akizungumza wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa Ripoti ya wachache kwenye kamati hiyo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu (kushoto), Machano Othman Said na Nassor Mazrui, wakizungumza jambo wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, akizungumza wakati alipokuwa akifafanua jambo wakati wa kikao cha bunge hilo cha kuwasilisha ripoti za Kamati 12 za bunge hilo leo.
Mjumbe wa Kamati namba 4 ya Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu, akizungumza wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa Ripoti ya wachache kwenye kamati hiyo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira wakizungumza jambo wakati wa kikao hicho. 
Mjumbe wa Kamati namba 6 ya Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu, akionesha moja ya nyaraka zinazoonesha utawala wa Zanzibar, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi wa Ripoti ya wachache kwenye kamati hiyo, mjini Dodoma leo. 
Mjumbe wa Kamati namba 6 ya Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu, akitoa ufafanuzi wa Ripoti ya wachache, wakati wa kuwasilisha Ripoti za Kamati 12 za bunge hilo, mjini Dodoma leo. 
Mjumbe wa Kamati namba 6 ya Bunge Maalum la Katiba, Ismail Jussa Ladhu, akitoa ufafanuzi wa Ripoti ya wachache, wakati wa kuwasilisha Ripoti za Kamati 12 za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakishangilia ufafanuzi wa Ripoti ya wachache iliyokuwa ikiwasilishwa na mjumbe wa Kamati namba 6, Ismail Jussa Ladhu kwenye kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Henry Shekifu, akitoa muongozo kwenye kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akitoa ufafanuzi kwenye kikao hicho kuhusu kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano kwa ajili ya kuondoa manung'uniko kwa wananchi wa pande zote.
Mwenyekiti wa Kamati namba 6 ya Bunge Maalum la Katiba, Stephen Wassira, akiwasilisha Ripoti ya wengei, wakati wa kuwasilisha Ripoti za Kamati 12 za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa Kamati namba 6 ya Bunge Maalum la Katiba, Stephen Wassira, akiwasilisha Ripoti ya wengei, wakati wa kuwasilisha Ripoti za Kamati 12 za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, wakijadili jambo wakati wa kikao hicho, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Raza (wa pili kushoto), akibadilshana mawazo na wajumbe wenzake, viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia (kushoto), Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mara baada ya kuaghirishwa kikao cha kuwasilisha Ripoti za Kamati 12 za bunge hilo, mjini Dodoma leo.

Na  Magreth Kinabo, Dodoma
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira amesema Serikali itawasilisha Hati ya Makubaliano ya Muungano katika  Bunge Maalumu la Katiba baada ya siku mbili zijazo.

Wassira ambaye  ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Sita (6) ya bunge hilo, ambazo zilikuwa zikijadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba, alitoa kauli hiyo leo, baada ya kuzuka mjadala juu ya uwepo wa hati hiyo na kama ipo kwa nini haijawasilishwa kwa wajumbe wa bunge hilo.

Mwenyekiti huyo, alitoa kauli hiyo, kabla ya kuanza kutoa taarifa za wajumbe walio wengi na wachache juu ya majadiliano ya sura hizo.

“Nataka kuwahakikishia kwamba Hati ya Muungano ipo tena ipo katika hali nzuri. Nataka kuahidi kwamba hati hiyo, itafikishwa katika Dola ya Jamhuri ya Muungano siku mbili zijazo,” alisema Wassira.

"Uwasilishaji wa Ripoti za Sura  ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Katiba, utaendelea hata kama bado hati hiyo haijawasilishwa".

Sitta alitoa kauli hiyo, baada ya mjumbe mmoja wa  Bunge hilo, John Mnyika kuomba mwongozo wa kutaka Bunge hilo, lisiendelee na mjadala wa sura hizo, hadi hati hiyo iwasilishwe Bungeni hapo.

“Mwenye mamlaka ya kutaka mjadala uendelee ni Kamati ya Uongozi ya  Bunge Maalum la Katiba, hilo analolisema Mnyika haliwezekani. Tunaliendesha Bunge hili kwa gharama. Ombi  hili litazuiliwa. Hati ya Makubaliano  itawasilishwa kwa wakati wake,” alisema Sitta huku akisisitiza kuwa hati hiyo haiwazuii kuendelea na kazi ya mjadala huo, hata Kanuni za Bunge hilo hazisemi hivyo.

Akiwasilisha maoni ya walio wengi katika kamati yake, Wassira alisema  wanapendekeza neno Shirikisho liondolewe kwa sababu Hati ya Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 ndio msingi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

”Hati ya Muungano ni sheria ambayo haikuanzisha shirikisho kama wajumbe walio wachache wanavyodai na badala yake ilikusudia kuanzisha Muungano. Hivyo, kutumia neno Shirikisho ni kwenda kinyume na Makubaliano yaliyopo katika Hati ya Muungano,” alisema Wassira.

Wassira  aliongeza kuwa  mapendekezo ya kuanzisha serikali ya shirikisho yanakinzana na masharti yaliyowekwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katika Sura 83 kifungu cha 9(2) kinachokazia uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

”Ingawa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inadai yalikuwa mawazo ya wananchi; swali ni kwamba kama wananchi walitoa maoni wangetaka kuvunja Muungano. Je Tume ingesemaje?. 

Shirikisho la serikali tatu litasababisha uendeshaji wa shughuli za umma kuwa  na gharama kubwa na hivyo kuwa mzigo wa kiuchumi kwa wananchi,” alisema.

Alisema, kwa mfano gharama za sasa za kuendesha taasisi za muungano ni takriban sh. Trilioni 10.7 kwa mujinbu wa makusanyo ya mapato yote ya ndani ni sh. Trilioni 12.6 kwa mujibu wa takwimu za bajeti ya mwaka wa fedha  2011/2012.

“Kuundwa kwa serikali ya muungano kutaongeza gharama na kupanua nakisi ya bajeti,” alisema.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa  wajumbe walio wengi wa kamati hiyo, wameshangazwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kudai kwamba muundo wa serikali tatu ni maoni ya wananchi walio wengi, wakati hakuna ushahidi wa takwimu.

“Mfumo wa serikali tatu pamoja na kupigiwa debe na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na UKAWA, lakini hakuna ushahidi wa takwimu kuonyesha kuwa unakubalika kwa wananchi walio wengi. Aidha, kwamba unakubalika na pande zote za Muungano,” alisema.

Wassira alisema kwa mujibu wa takwimu za Tume, Zanzibar asilimia 61 inasemekana walitaka Muungano wa Mkataba; asilimia 31 walitaka muundo wa serikali mbili.

“Katika hali hiyo kusema serikali tatu ni mawazo ya wananchi walio wengi wa wapi? Kwa Tanzania Bara kati ya watu 16,000 waliochangia Muungano, 8,682 ni kutoka Mkoa wa Kigoma pekee na waliosalia ni kutoka mikoa mikoa mingine iliyobaki.”

“Sasa kwa takwimu hizi unawezaje kusema watu wengi wanataka serikali tatu? Suala la msingi hapa ni kwamba mfumo wa kukusanya maoni uliotumiwa na Tume bila ya kujali ukubwa au udogo wa sampuli, hauna mamlaka ya kubadili mfumo kutoka Muungano kuwa Shirikisho,” alisema Wassira.

Aliongeza: “Hii ni kweli, kwa vile mwaka 1964 Rais Julius Nyerere aliwawakilisha Watanganyika na Rais Abeid Amani Karume aliwawakilisha Wazanzibar wote katika makubaliano ya kuunganisha nchi zetu mbili.”

Wassira alisema kubadilisha hati ya muungano unahitaji kwanza kurudisha Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, kisha kupitia kura ya maoni, uamuzi wa mfumo gani wa Muungano na kama ni shirikisho, basi viongozi wa Tanganyika na Zanzibar wajadiliane aina ya ushirikiano.

Katika Kamati hiyo, Wassira aliwasilisha maoni ya wajumbe wachache,ambao  walipendekeza Muungano wa Tanganyik na Zanzibar uwe wa Shirikisho.


Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Kamati Namba Saba  ya Bunge hilo,kuhusu Sura ya Kwanza nay a Sita, ya Rasimu ya Katiba ,BrigediaJenerali Mstaafu Hassan Ngiwilizi  aliwasisha maoni ya kamati yake,ambayo pia wajumbe wengi walipendekeza muundo wa Serikali Mbili na  maoni ya wajumbe wachache walipendekeza Muundo wa Shirikisho  lenye Serikali Tatu.

No comments:

Post a Comment