Magari
mapya yenye thamani ya shilingi million
280, yaliyonunuliwa kwa ajili ya kuboresha mfumo wa usafirishaji katika
jiji la Dar es salaam yakiwa
kwenye yadi ya Posta tayari kwa ajili ya
kuhakikisha kuwa mtumaji wa barua,
vifurushi na vipeto
vinavyotumwa na wateja vinawafikia wahusika siku hiyo hiyo
aliyotuma.
Magari
mapya yaliyonunuliwa na Shirika la Posta Tanzania na kuzinduliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuboresha
huduma za ukusanyaji na usambazaji wa barua na vifurushi jijini Dar es Salaam
yakiwa kwenye yadi ya shirika hilo.
Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa Biashara, Fortunatus Kapinga (kulia), akimkabidhi moja ya kadi za magari mapya ya kuboresha huduma za ukusanyaji na usambazaji kupitia mtandao wa Posta wa barua, Meneja Msaidizi Huduma za Barua mkoani Dar es Salaam, Hamis Mchangila, mara baada ya kuyazindua jijini mwishoni mwa wiki.
Meneja Mkuu wa Uendeshaji Biashara za Posta Bw. Fortunatus Kapinga, akilijaribu kuendesha moja kati ya magari hayo, wakati wa uzinduzi rasmi jijini juzi.
Meneja
Mkuu wa Uendeshaji Biashara, Bw. Fortunatus Kapinga (kulia), akimkabidhi funguo za moja ya
magari mapya Meneja Msaidizi wa Huduma
za barua, mkoa wa Dar es Salaam Bw. Hamis
Mchangila mapema juzi. Magari hayo, yatatumika kuboresha mfumo wa ukusanyaji na usambazaji wa barua, vifurushi
na vipeto jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa Biashara za Posta Bw. Fortunatus Kapinga, akitoa maelekezo
kwa Maofisa na madereva wa Posta mara baada ya kukabidhi magari hayo, kwa
uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi wa Huduma za barua mkoani Dar es Salaam, Bw. Hamis Mchangila, akilijaribu kuendesha moja kati ya magari aliyokabidhiwa na Meneja Mkuu wa Uendeshaji wa Biashara, Fortunatus Kapinga, jijini juzi. (Picha zote na mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment