TANGAZO


Saturday, March 1, 2014

Wananchi wajitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Taifa mjini Zanzibar



Wananchi wa maeneo ya Mtoni, mjini Unguja, wakiwa wamejitoleza katika zoezi la Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa, katika Viwanja vya Shule ya Mto Pepo, Wilaya ya Magharibi Unguja. Zoezi hilo linafanyika kwa nchi nzima kuandikishwa wananchi ili kuweza kupata vitambulisho hivyo.
Wananchi wakiwa katika viwanja vya Shule ya Mto Pepo, mjini Unguja, wakijiandikisha kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
Ofisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Tanzania, akitaja majina ya wananchi waliokuwa tayari wameshafanyiwa usaili na kufuata hatua nyengine ya upigaji picha.
Mwananchi akikamilisha taratibu za usajili kwa ajili ya kupatiwa Kitambulisho cha Taifa.
Ofisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, akitaja majina ya wananchi waliokamilisha kujaza fomu na kuchukua hatua ya upigaji wa picha za vitambulisho hivyo.
Ofisa wa vitambulisho vya Taifa, akijaza fomu ya mmoja wa wananchi katika hatua ya picha.
Ofisa vitambulisho vya Taifa, akitayarisha vifaa vya upigaji picha kwa ajili ya kuanza kazi hiyo mara moja.
Wananchi wakihojiwa na Makarani wa Vitambulisho vya Taifa na kujaza fomu maalum kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa, kwenye viwanja vya Mto Pepo Chumbuni, mjini Unguja jana. 
Wananchi wa Mto Pepo mjini Unguja wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa, maeneo ya Mto Pepo, mjini Unguka jana. (Picha zote kwa hisani ya Zanzi News blogspot.com)

No comments:

Post a Comment