TANGAZO


Saturday, March 1, 2014

Bodi ya Dawa na Vipodozi Zanzibar yakubaliana na mfanyabiashara aliyeingiza mchele mbovu aurejeshe ulikotoka nchini Pakistan



Mfanyabiasha aliyeingiza mchele kutoka Pakistan, ambao umegundulika kuwa ni mbovu na haufai kwa matumizi ya chakula kwa Binaadamu, Mohammed Mauly, akizungumza na waandishi wa habari, mjini Zanzibar jana kuhusu kukubaliana na Bodi ya Dawa na Vipodozi kuurejesha nchini Pakistani, alikoutoa na kueleza kuanza kwa zoezi la matayarisho hayo mara moja.
Mchele mbovu uliothibitishwa na Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi Zanzibar,  ukiwa kweye ghala la Mwanakwerekwe, ukisubiri kurejeshwa nchini Pakistan ulikonunuliwa.
Wachukuzi, wakipakia mchele kwenye gari kwa ajili ya kuusafirishwa kurejeshwa ulikotoka nchini Pakistani.
 
Mfanyabiashara aliyeingiza mchele mbovu kutoka Pakistani Mohamed Mauly, akionesha mchele huo, uliothibitishwa na Bodi ya vyakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar na mwenyewe kuridhika na majibu hayo, na kusema sio aliouagiza, hivyo kupeleka madai na kutakiwa aurudishe ili aweze kupewa haki zake na Kampuni ya Bilal Rice Mills ya Pakistan. (Picha zote na Makame Mshenga wa Maelezo-Zanzibar)

No comments:

Post a Comment