TANGAZO


Thursday, March 27, 2014

TBS yawafunda walemavu wa usikivu (Viziwi) kutoka Mikoa ya Dodoma na Singida, Tabora na Shinyanga

Meza kuu ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi wakiwashangilia kwa lugha ya alama wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (hawapo pichani) wakati wakijitambulisha kwenye semina iliyoandaliwa na TBS kwa ajili ya kuwafunda walemavu hao masuala ya viwango vya ubora katika shughuli za,uzalishaji  iliyofanyika mapema juzi Jumatatu Machi 24, 2014. (Picha zote na John Banda)
Ofisa uhusiano wa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania ndg. Nicholaus Lubinga (aliyesimama nyuma) akizungumza jambo kwa lugha ya alama wakati wa semina  ya masuala ya viwango vya ubora kwa wwjasiriamali wenye ulemavu wa kusikia iliyoandaliwa na TBS ambayo imefanyika leo mjini Dodoma.
Mkuu wa mkoa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiwasisitizia walemavu wasiosikia (viziwi) kuzingatia ubora wa viwango kwenye bidhaa wanazozalisha kwenye sekta ya kilimo, ufugaji nyuki na mifugo na ujasiriamali ili kunufaika na masoko ya kimataifa wakati akifungua semina kwa walemavu hao juu ya masuala ya ubora wa viwango  iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS, semina hiyo ilifanyika leo mjini Dodoma, wengine pichani ni maafisa kutoka TBS.
Wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (viziwi), wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, mifugo na nyuki na ujasiriamali kutoka Mikoa ya Dodoma singing, tabora na shinyanga wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa Dodoma na kutafsiriwa kwa lugha ya alma wakati wa ufunguzi wa semina ya masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na kufanyika juzi, mjini Dodoma .
Baadhi ya wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) wanaojihusisha na shughuli za uzalishaji katika sekta za kilimo, ufugaji mifugo na nyuki na ujasiriamali kutoka mikoa ya Dodoma, singida,Tabora na shinyanga wakishangilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa na mkuu wa mkoa Dodoma na kutafsiriwa kwa lugha ya alama kwenye semina ya masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS mapema juzi, mjini Dodoma.
Picha ya pamoja baina ya mkuu wa mkoa wa dodoma Dk. Rehema Nchimbi, wataalamu wa masuala ya viwango vya ubora kutoka TBS na walemavu wasiosikia (viziwi) kutoka mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga muda mfupi baada ya mkuu huyo wa mkoa kufungua semina kwa walemavu hao juu ya  masuala ya ubora wa viwango iliyoandaliwa na shirika la viwango tanzania TBS na kufanyika mapema juzi Jumatatu Machi 24, 2014.

No comments:

Post a Comment