Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakielekea ukumbini kwa ajili ya kikao cha mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Joshua Nasari, akila kiapo kabla ya kuwasilishwa mapendekezo ya mabadiliko ya Kanuni za 37 na 38 za bunge hilo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akila kiapo kabla ya kuwasilishwa mapendekezo ya mabadiliko ya Kanuni za 37 na 38 za bunge hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho, akiwasilisha mapendekezo ya Kanuni za 37 na 38 yanayowataka wajumbe wa bunge hilo kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja wakati wa maamuzi ya suala moja linatakiwa kutolewa maamuzi ya kupiga kura wakati wa utungaji wa Katiba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni, Pandu Ameir Kificho, akiwasilisha mapendekezo ya Kanuni za 37 na 38 katika kikao hicho.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose Migiri (kulia), akiwa na Naibu wake, Angela Kairuki, wakati wa kikao hicho.
Ukumbi wa Bunge ulivyokuwa ukionekana wakati wa kuwasilishwa kwa mapendekezo hayo na kamati hiyo katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika, akitoa hoja ya kupinga pendekezo la kupiga kura ya siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika, akielezea hofu yake iwapo pendekezo la kupinga kura ya siri na wazi itatumika kwa wakati mmoja katika kuamua suala moja kwenye bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, John Mnyika, akionesha moja ya nyaraka iliyovuja, aliyoitaja kuwa ni ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwashinikiza wanachama wake kwamba atakayekiuka maagizo ya kulipigia kura ya ndio suala la Serikali mbili atashughulikiwa na chama hicho na kwa hivyo kujenga hoja kwamba kwa kuruhusu kura hizo mbili zipigwe, itawalazimisha wajumbe wa chama hicho kutokupiga kura kwa ridhaa za nafsi zao na hivyo kulazimika kupiga kura kwa shinikizo la chama chao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda, akiunga mkono pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akichangia na kupinga pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohammed Aboud Mohammed, akichangia na kuunga mkono pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akichangia na kupinga pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwalimu Oluochi akichangia na kupinga pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mohamed Raza, akichangia na kubali pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Esther Bulaya, akichangia na kukubali pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Joshua Nasari, akichangia na kupinga pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakishangilia hoja zilizokuwa zikitolewa na wachangiaji mbalimbali katika pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akichangia hoja hiyo kwa kupendekeza kuwa Kamati ya Mashauriano na Maridhiano zikutane kwa ajili ya kuamua suala hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Machari, akichangia na kupinga pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo na pia kuwatuhumu baadhi ya wajumbe kuwahonga wajumbe wenzao ili kuwaunga mkono katika masuala ya maamuzi kwenye bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, mmoja wa watuhumiwa wa masuala hayo, akikanusha suala hilo na pia kumtaka mjumbe Machari kumuomba radhi katika tuhuma zake hizo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Askofu Donald Mtetemela, akiwataka wajumbe wa bunge hilo kuwa na nidhamu wakati wa kuchangia mambo mablimbali yanayowasilishwa kwenye bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, akichangia na kupinga pendekezo la kupiga kura za siri na wazi kwa wakati mmoja, lililopendekezwa na kuwasilishwa na Kamati ya Kanuni za bunge hilo.
No comments:
Post a Comment