Bondia Hamisi Mputeni (kushoto), akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Victor Njaiti, wakati wa mpambano wao, katika mashindano ya Klabu bingwa Mkoa wa Dar es Salaam jana. Njaiti alishinda kwa pointi. (Picha zote kwa hisani ya www.superdboxingcoach.blogspot.com) |
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya MMJKT jana imeibuka mabigwa wa mashindano ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuvipiku vilabu nane vilivyojitokeza kushiriki katika mashindano hayo na kutawazwa kuwa bingwa wa Mkoa.
Baadhi ya mabondia waliocheza fainal za mashindano hayo ni Hamisi Mrisho wa 'MMJKT' aliyesambaratishwa kwa pointi na bondia Oscar Richard wa 'Urafiki' na Omari Mohamed wa Urafiki aliyechezea kichapo kutoka kwa mwenziwe John Mwambinga na bondia anaekuja kwa kasi ya hali ya juu akitokea timu ya Ashanti ya Ilala kwa sasa akichezea timu ya 'MMJKT', alifanikiwa kumpiga John Christian wa 'Mgulani' naye Saleh Abdallah wa Mgulani alishindwa kutamba mbele ya Undule Langson wa Magereza.
Jacobo Agusteno wa Mgulani, alishindwa kufurukuta mbele ya Bosco Bakari wa 'MMJKT' katika mpambano mwingine uliowakutaniasha Festo Ngabo wa Magereza alishindwa kutamba mbele ya Victor Njaiti wa MMJKT, naye bondia Mohamedi Chibumbuli wa Magereza akampiga vibaya Said Saleh wa Mavituzi.
Akizungumzia maandalizi ya mabondia wa Mkoa, Mwenyekiti wa Chama cha Ngumi Mkoa wa Dar es salaam 'DABA' Akaroli Godfrey amesema kwamba, sasa mabondia wa timu ya Mkoa wa Dar es Salaam wapo kambini wakijiandaa na mashindano ya majiji yatakayoanza Kampala Uganda April 2 mwaka huu.
Timu hiyo ambayo ipo chini ya makocha wazoefu wakiongozwa na David Yombayomba, Ferdnand Nyagawa, mazoezi yake yanayofanyika kila siku katika kambi ya Mgulani JKT, wakisaidiwa na Mazimbo Ally na Kameda Antony.
Timu hiyo, ina maitaji mbalimbali yakiwemo kambi pamoja na kupeleka timu Uganda ambayo itagharimu milioni 16 kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano hayo ambapo mpaka sasa wameendaa sehemu mbalimbali ikiwemo makampuni na kwa watu binafsi.
Hata hivyo, hakuna mafanikio yoyote, hivyo kuwaomba wadau wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kusaidia timu hiyo, ambayo inakabiliwa na mashindano ya majiji kwa sasa.
No comments:
Post a Comment