Papa Francis
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ametetea
rekodi ya kanisa hilo katika utatuzi wa suala la unyanyasaji wa watoto
unaofanywa na mapadri.
Katika mahojiano na gazeti moja la Italia, Papa Francis amesema kuwa hakuna
aliyefanya zaidi kutatua swala hilo kuliko uongozi wa kanisa hilo.Amesema kuwa kanisa hilo limewajibika katika kuchukua hatua za uwazi, lakini ndio taasisi inayoshambuliwa.
Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulishtumu, utawala wa Vatican kwa kushindwa kukabiliana na suala la unyanyasaji wa watoto mbali na kuwaficha wanaotekeleza tendo hilo.
No comments:
Post a Comment