Huduma za usafiri jijini Nairobi zimekwama kufuatia hatua za
wenye magari kugoma hii leo wakilalamikia nyongeza ya ada ya kuegesha magari
jijini humo.
Maelfu ya wafanyakazi wamelazimika kutembea kwa miguu na wasafiri wa kutoka
jijini kwenda maeneo ya mashambani nao kulazimika kuahirisha safari zao."Juzi tulikuwa na Gavana Evans Kidero na tukakubaliana kiasi tunachopaswa kulipa lakini jana tulipofika wafanyakazi wa kaunti wakakataa kiasi tulichokuwa nacho," Bwana Kariuki alisema.
Kaunti hizo mpya hata hivyo zimejikuta njia panda baada ya kupata madaraka bila fedha za kuandamana nayo; ambapo zimelazimika kuongeza kodi kama njia mojawapo ya kujiimarisha kiuchumi.
Mkuu wa polisi nchini Kenya, David Kimaiya aliagiza idara ya trafiki nchini Kenya kunasa magari yote yaliyofunga barabara za mji.
No comments:
Post a Comment