Muungano wa Ulaya, EU, umetangaza ufadhili wa dola billioni 15
kwa Ukraine katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Rais wa tume ya Muungano huo Jose Manuel Barrosso, amesema kuwa mkopo huo ni
miongoni mwa ahadi za EU kuisaidia serikali mpya ya Ukraine kuimarisha uchumi
wake.Tayari serikali ya Marekani imeahidi kuipatia Ukraine mkopo mwengine wa dola bilioni moja.
Waziri mkuu nchini Urusi, Sergei Lavrov, amesema kuwa mamlaka nchini Ukrain na yale ya Jimbo la Cremia, yataamua iwapo yatahitaji wachunguzi wa kimataifa katika taifa hilo kama ilivyopendekezwa na Rais Obama ili kusaidia kukwamua mzozo huo
Urusi haitokubali ghasia Ukraine
Mazungumzo ya Bwana Lavrov mjini Madrid, ni miongoni mwa misururu ya mikutano ya wanadiplomasia wakuu inayonuia kusitisha hali ya wasiwasi nchini Ukraine, ambapo wanajeshi wa Urusi pamoja na wale wanaounga mkono Urusi katika jimbo la Cremia wameuteka mfereji wa Cremia.
Lakini kufikia sasa Lavrov, amekuwa akikwepa swala hilo na kusema kuwa ni haki ya serikali ya Ukrain kuamua iwapo inahitaji wanajeshi wa kulinda amani nchini humo, pendekezo lililotolewa na Marekani kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanajeshi wa Urusi wameondoka nchini humo.
Katika mikutano yake hii leo Bwana Lavrov huenda akaagiza kubuniwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Ukrain huku marekebisho ya kikatiba yakihudumia maslahi ya majimbo yote nchini Ukrain,na hivyo basi kutoa fursa kwa maeneo yaliyo na raia wanaozungumza lugha ya Urusi kuwa na ushawishi mkubwa mbali na kupewa ulinzi wa kutosha.
No comments:
Post a Comment