TANGAZO


Wednesday, March 5, 2014

Mapigano mapya mjini Juba

 Wanajeshi wa waasi nchini Sudan Kusini

Wanajeshi watano wa serikali ya Sudan Kusini wameuawa kufuatia mapigano makali ndani ya kambi moja ya kijeshi mjini Juba.
msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema kuwa wanajeshi wengine watatu walijeruhiwa kwenye mapigano hayo iliyotokea katika kambi ya jeshi ya Jebel.
Mapigano kama hayo ndani ya kambi hiyo kati ya makundi hasimu yalisababisha mgogoro mkubwa wa kisiasa nchini humo.
Mkaazi mmoja wa Juba ameiambia BBC, kwamba moshi mweusi ulionekana ukitapakaa angani juu ya kambi hiyo karibu na chuo kikuu cha Juba na kwamba watu wameonekana wakilitoroka eneo hilo.
Akiongea muda mfupi kwenye runinga ya taifa muda mfupi baada ya mapigano hayo kuanza, Brigadier General Malak Ayuen Ajok amesema kuwa waliouwa ni wanajeshi waatiifu kwa serikali.
Amesema mapigano hayo yalisababisha na mvutano kati ya wanajeshi ambao walikuwa wakizozana kuhusu kucheleweshwa kwa mishahara yao.
Ajok, ameongeza kuwa hakuna dalili yoyote ya mapigano hayo kusambaa katika maeneo mengine ya mji huo.
Lakini watu wengi wanaoishi karibu na kambi hiyo ya wamekimbia makwao na kutafuta hifadhi katika piga makanisa na shule.
Mzozo wa Sudan kusini ulianza mjini Juba, mnamo mwezi Disemba mwaka uliopita kufuatia hali ya wasiwasi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar lakini ukaenea kote nchini humo.

No comments:

Post a Comment