Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa na wafuasi wa chama chake, huku wakinyeshewa na mvua katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Wenda, Kata ya Mseke, Iringa Vijijini leo. (Picha zote na Kamanda wa Matukio Blog)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa akiwasalimia wafuasi wa chama hicho, alipokuwa akiondoka baada ya kumalizika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Wenda, Kata ya Mseke, Iringa Vijijini leo.
Mgombea Ubunge, Godfrey Mgimwa akijipigia chapuo ya kura katika Kijiji cha Sadani, Kata ya Mseke leo.
Mfuasi wa CCM, akishangilia wakati mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke, Iringa Vijijini leo.
Mgimwa akiwapungia wananchi huku akiwa amebebwa katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke, Iringa Vijijini leo, wakati wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Kalenga.
Mfuasi wa CCM, akishangilia huku akiwa amembeba mtoto mgongoni, wakati mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke, Iringa Vijijini leo.
Furaha ya wananchi kwa Mbunge wao mtarajiwa wa Kalenga ilikuwa ni kumbeba mgombea huyo.
Wananchi wakisikiliza hotuba ya mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa, alipokuwa akijinadi katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Wenda, ambao licha ya kutawaliwa na mvua lakini ulifana.
Mgombea Ubunge wa Kalenga, Godfrey Mgimwa akihutubia na kuwaomba kura wananchi katika mkutano wa kampeni ambao ulitawaliwa na mvua kubwa katika Kijiji cha Wenda. |
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu akihutubia wananchi kwa kumnadi Mgimwa katika Kijiji cha Sani, Kata ya Mseke leo. |
Msanii wa muziki na filamu, Ummy Wenslaus "Dokii' akicheza na mama wa Kimasai, wakati wa kampeni za kumnadi Mgimwa katika Kijiji cha Tanangozi, Kata ya Mseke leo jioni |
No comments:
Post a Comment