Baadhi ya waandishi wa habari wakitekeleza
majukumu yao leo jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania inaungana na nchi nyingine
za Afrika wanachama wa Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) katika
kuadhimisha siku ya APRM na kutoa
taarifa ya tathmini ya Utawala bora nchini. (Picha zote na Eleuteri
Mangi -MAELEZO)
Na
Frank Mvungi-MAELEZO
MPANGO
wa Afrika wa kujitathmini kiutawala bora (APRM) umebainisha kuwa Tanzania ni
moja ya Nchi zinazofanya vizuri katika utawala
bora.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania Rehema Twalib wakati wa mkutano
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam alipokuwa akieleza mafanikio
yaliyofikiwa hadi sasa ikiwa ni sehehmu ya maadhimisho ya siku mchako huo ambayo
huadhimishwa Machi 9 kila mwaka.
Bi. Rehema alibainisha kuwa Tanzania imepata mafanikio katika Nyanja za Demokrasia
na Utawala Bora, Siasa, Usimamizi wa uchumi, uendeshaji wa makampuni,Maendeleo
ya uchumi-Jamii na Masuala mtambuka kama afya.
Wakati
huo huo alizitaja hatua zinazochukuliwa na Serikali kuwa ni kuanza kufanyia
kazi mpango kazi wa kitaifa (NPoA) wa kuondoa changamoto zilizobainishwa katika
ripoti ya APRM kuhusu hali ya utawala bora nchini.
Pia
Bi. Rehema alizitaja hatua nyingine ambazo Tanzania imefikia katikakutekeleza mchakato wa APRM kuwa ni kuwashirikisha
wananchi kutoa maoni yao kuhusu hali ya utawala bora nchini na Serikali
kuruhusu wataalamu wa utawala bora kutoka nchi wanachama kuja nchini kuhakiki
mchakato huo.
Aidha,
Bi. Rehema alibainisha kuwa lengo kuu la mpango huu ni kuwashirikisha wananchi
ili kushirikiana na Serikali zao kubaini changamoto za utawala bora ili
zifanyiwe kazi na kuhimiza nchi kutekeleza viwango vinavyokubalika kimataifa na
kikanda.
APRM
ni mpango ulioasisiwa machi 9, 2013 na wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU)
ambapo Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54 za AU zilizokwisha
jiunga na mpango huu ambapo ilijiunga mwaka 2004.
No comments:
Post a Comment