TANGAZO


Thursday, March 20, 2014

Msaii maarufu wa Filamu nchini, Yussuf Mlele, atoa msaada wa vifaa vya masumbwi

Msanii wa filamu nchini, Yusuph Mlela (kushoto), akikabidhi vifaa mbalimbali kwa kocha wa klabu ya Msisiri Daudi Muhunzi ikiwa ni uboreshwaji wa klabu hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni, Dar es alaam katikati ni mdau wa mchezo huo Ally Moja. (Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com) 
Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela kushoto akikabidhi vifaa mbalimbali vya mchezo wa ngumi kwa kocha wa klabu ya Msisiri Daudi Muhunzi ikiwa ni uboreshwaji wa klab hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni Dar es salaam  wa pili kulia ni Ally Moja na Rashid Kipaga
 
Msanii wa filamu nchini Yusuph Mlela (kushoto), akikabidhi,  vifaa mbalimbali vya mchezo wa ngumi kwa kocha wa klab ya Msisiri Daudi Muhunzi ikiwa ni uboreshwaji wa klab hiyo iliyopo CCM Msisiri Kinondoni Dar es salaam  wa pili kulia ni Ally Moja na Rashid Kipaga
. 
Na Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu za bongo, Yusuph Mlela ameibukia katika mchezo wa masumbwi nchini kwa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo huo.
 
Vifaa alivyokabidhi ni pamoja na Glove, Clip bandeji, Protekta, Gum Shit kwa klabu ya Msisiri iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa hivyo Mlela alisema nimevutiwa na vijana wenzangu jinsi wanavyojituma kufanya mazoezi hivyo nikaamua kujitolea kidogo nilicho nacho kwa ajili ya kuendereza mchezo huu wa masumbwi
 
Katika Kata yangu, ambapo mimi naishi karibu na maeneo haya hivyowalivyo niomba nichangie nikawa sina jinsi kwa kuwa na mimi mwenyewe siku moja moja nitakuwa nakuja kufanya mazoezi hapa hapa nawaomba wadau wengine wenye uwezo zaidi yangu ata ambao wapo kama mimi wasaidie vijana kwa ajili ya kujiendeleza na mchezo huu waupendao.
 
Naye kocha wa mchezo wa ngumi katika Klabu ya Msisiri Daudi Muhunzi alitoa shuklani zake kwa Mlela kuwakumbuka vijana wenzie ambao walikuwa na huaba wa vifaa vya ngumi kwani yeye amekuwa kama mkombozi katika kata hiyo.
 
Aliongeza kwa kusema tunaomba wadau wengine waje watusaidie vifaa mbalimbali kama punch bag,pad na maswala ya hudhamini wa  muda mrefu   kwa ajili ya kuendereza gym hii ambayo tunaitumia kwa kuchangia kidogo  

No comments:

Post a Comment