*Mangula atoa somo la upigaji kura mkutanoni
*Awataka wananchi (wapigakura), wasije wakaharibu ama kupoteza kura zao
|
Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia kwa furaha walipokuwa wakimlaki mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa (hayupo pichani), katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini jioni leo. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog) |
|
Mfuasi wa CCM, akiwa mbele ya Polisi, huku akionesha picha ya mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini leo jioni. |
|
Mgombea Godfrey Mgimwa, akiwa amebebwa juu alipowasili katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kalenga jioni leo. |
Wafuasi wa CCM, wakishangilia huku wakiwa na picha za mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ipamba, Kata ya Kalenga, Iringa Vijijini leo.
|
Ni furaha iliyoje katika mapokezi ya Mgimwa, wananchi na wanachama wa CCM wa Kijiji cha Ipamba, Tosamaganga, wakiserebuka wakati wa mapokezi ya mgombea wa chama hicho, Godfrey Mgimwa leo. |
Msanii mahiri wa filamu na muziki, Ummy Wenslaus 'Dokii" akihamasisha wakati wa mkutano wa kampeni za CCM katika Kijiji cha Ipamba, Tosamaganga leo.
|
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, akipokea kadi kutoka kwa mwanachama wa Chadema, Said Mbilinyi aliyeamua kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Ipamba, jimboni Kalenga leo. |
|
Diwani wa Kata ya Kalenga, Ameria Galinoma akionesha ishara ya dole baada kufurahishwa na hotuba ya mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, kupitia CCM, Godfrey Mgimwa leo. |
|
Sista aliyewahi kumfundisha marehemu Dk. William Mgimwa darasa la tatu na la nne katika Shule ya Wassa, Paula Msambwa akikumbatiana kwa fura na mtoto wa marehemu Mgimwa, mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa. |
|
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa, akisalimiana na Sista Paula Msambwa (73), aiyewahi kumfundisha babake, mrehemu Dk. William Mgimwa daras la tatu na la nne katika Shule ya Wassa kati ya mwaka 1964-1965. Mgombea huyo, alikutana naye wakati wa kampeni katika Kijiji cha Tosamaganga, Kata ya Kalenga, Iringa Vijijini. |
|
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akihutubia katika mkutano wa kampeni za CCM, Jimbo la Kalenga katika Kijiji cha Tosamaganga, ambapo alihimiza amani siku ya kupiga kura na kuwataka wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho kutokupoteza ama kuharibu kura zao bali wampigie kijana wao, Godfrey Mgimwa, ili aweze kuwaletea maendeleo jimboni mwao humo katika kuendeleza kazi aliyoifanya baba yake, marehemu Dk. Mgimwa. |
|
Mapokeszi ya Mgimwa katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kalenga leo. |
|
Umati wa wananchi na wanachama wa CCM, wakiserebuka kwa kuimba na kucheza wakati wa mapokezi ya mgombea wa chama hicho leo. |
|
Ni furaha kwa kwenda mbeleeeeeee, hivi ndivyo ilivyokuwa katika mapokezi ya mgombea huyo leo. |
|
Diwani wa Kata ya Kalenga, Ameria Galinoma (kulia) na Diwani wa Viti Maalumu wa Kata hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT, Wilya ya Iringa Vijijini, Shakila Kiwanga pamoja na wananchi wakishangilia katika mkutano wa kampeni za CCM katika Kijiji cha Kalenga leo. |
|
Dokii akifanya vitu vyake katika mkutano wa kampeni za CCM Kalenga mjini leo. |
|
Doria ikiwa imeimarishwa katika Jimbo la Uchaguzi la Kalenga, wakati wa mkutano wa chama hicho leo. |
|
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akionesha fomu ya mfano ya kupigia kura yenye picha za wagombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini leo. Uchaguzi utafanyika Jumapili Machi 16, mwaka huu. |
Mgombea Godfrey Mgimwa (katikati), akiserebuka pamoja na wananchi na wanachama wa chama hicho, wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment