TANGAZO


Monday, March 10, 2014

Bunge Maalum la Katiba Dodoma leo

*Maelewano suala la kupiga kura bado
*Wajumbe wataka rasimu ipitishwe ikiwa imekamilika

Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, Profesa Costa Mahalu, akizungumza jambo na mjumbe wa kamati hiyo, Tundu Lisu (kushoto), wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo. Hata hivyo bunge hilo liliaghirishwa kutokana na baadhi ya wajumbe kudai kwanza masuala yote yanayohusu vipengele vya Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, vya 37 na 38 vinavyohusu suala la upigaji kura, vikamilike ndipo hoja ya kuipitisha iwasilishwe kwa ajili ya kuipitisha. Baadhi ya wajumbe walisema suala la kupitishwa vipengele hivyo sio lazima kwa sasa kwani kamati ya Kanuni na ya Ushauri bado zitakuwepo kwa ajili ya kuendelea kufanya mabadiliko yatakayohitajika wakati wa kuandaa vipengele vya Katiba, huku hoja hiyo, ikitiliwa nguvu na Kamati ya Rasimu ya Kanuni za bunge hilo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda na Mohamed Seif Khatiba, wakizungumza jambo, wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Dk. John Magufuli (kushoto), Hezekia Oluoch, Abdallah Bulembo na Dk. Emmanuel Nchimbi, wakijadili jambo kwenye viwanja vya Bunge kabla ya kuingia kwenye kikao cha bunge hilo. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Dominick, Lyamchay, Hussein Salum na Salim Ally, wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kushoto) na Samwell Sitta, wakijadili jambo ndani ya ukumbi wa bunge kabla ya kikao cha bunge hilo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Muhagama (kulia), akiwaeleza jambo wajumbe wenzake wa bunge hilo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kushoto) na Almasi Maige, ndani ya ukumbi wa bunge hilo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba (kulia), akiwaeleza jambo wajumbe wenzake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda (wa pili kulia), Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na Steven Wasira, mara baada ya Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, kuaghirisha kikao cha bunge hilo leo kutokana na wajumbe wa bunge hilo, kusubiri nakala za Rasimu ya Kanuni za bunge hilo kwa ajili ya kuipitisha ili iweze kutumika rasmi katika vikao vya Bunge katika kuandaa Katiba hiyo.

No comments:

Post a Comment