TANGAZO


Saturday, February 15, 2014

Viwanja vya ndege vyafunguliwa indonesia

Mlipuko wa volkano

Viwanja kadhaa vya ndege vimefunguliwa katika kisiwa cha Indonesia cha Java baada ya kulazimishwa kufungwa na wingu kubwa la jivu la volkano.
Mlipuko huo wa mlima Kelud ulisababisha zaidi ya watu laki mbili kuyahama makaazi yao .
Mlima huo sasa umetulia na kwamba hali ya hewa katika eneo la Java imeimarika,licha ya vumbi la mlipuko huo kutapakaa mamia ya kilomita kadhaa kutoka kwenye mlima huo .
Makumi ya maelfu ya wakaazi wanaendelea kuishi katika kambi za mda na kwamba wanakabiliwa na uhaba wa mablanketi,dawa na maziwa ya watoto.
Kufikia sasa haijabainika ni lini raia hao wateweza kurudi katika makao yao.

No comments:

Post a Comment