Wizara ya maswala ya ndani nchini Bahrain imesema kuwa polisi mmoja aliyejeruhiwa katika mlipuko siku ya ijumaa ameaga dunia.
Polisi mwingine mmoja alijeruhiwa.
Mlipuko huo ulitokea katika kijiji cha watu wa dhehebu la shia cha Dair nje ya mji mkuu wa Manama wakati wa maandamano.
Afisa mwengine wa Polisi pia alijeruhiwa na mlipuko huo huku mlipuko mwengine ukisababisha uharibifu mdogo katika basi moja lililokuwa likibeba mafisa wa polisi katika kijiji chengine cha Bahrain.
Maandamano hayo yanaadhimisha miaka mitatu tangia kuzuka kwa maasi miongoni mwa watu wa dhehebu la Shia wa nchini Bahrain walio wengi wanaotaka utawala wa kifalme katika taifa hilo linaloongozwa na watu wa dhehebu la sunni.
No comments:
Post a Comment