Vifaa kwa ajili ya Timu za Mikoa ya Unguja Mitatu Mkoa wa Kusini , Kaskazini na Mjini Magharibi, utaunda timu za Mikoa kuchuana na Mikoa ya Tanzania Bara kutafuta vipaji vya wachezaji watakaounda timu ya Taifa ya Tanzania. (Picha zote kwa hisani ya ZaziNews Blog)
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA Ravia Idarous. kulia akimkabidhi Vifaa kwa timu ya Mkoa wa Kusini Unguja Ali Yussuf, kwa ajili ya timu yao kuweza kutumia katika michuano hiyo, yanayotarajiwa kuaza
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA Ravia Idarous. kulia akimkabidhi Vifaa kwa timu ya Mkoa wa Kusini Unguja Ali Yussuf, kwa ajili ya timu yao kuweza kutumia katika michuano hiyo, yanayotarajiwa kuaza
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira Zanzibar ZFA, Ravia Idarous. kulia akimkabidhi Vifaa Kiongozi wa timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi Ahmada Haji,kwa ajili ya timu yao kuweza kutumia katika michuano hiyo, yanayotarajiwa kuaza Febuari 22-2-2014.
Mwenyekiti wa ZFA Taifa Ndg. Ravia Idarous, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na kuazishwa kwa michuano ya Kukuza Vipaji kwa Wachezaji wa Tanzania katika kukuza Timu ya Taifa ya Tanzania, kupitia michuano hiyo kuweza kuchagua wachezaji wenye vipaji kutoka katika timu za Mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar, Jumla ya Mikoa 32 itashiriki michuano hiyo inayotarajiwa kuaza 22-2-2014. ilimkuweza kuibua vipaji kwa vijana.
Viongozi wa ZFA Taifa wakifuatilia hafla hiyo ya makabidhiano ya Vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Kampuni ya TBL, ili kuweza kuibua Vijana vya Vijana kuund timu ya Taifa ya Tanzania kwa maandalizi ya Michuano ijayo, ili Tanzania ishiriki vizuri katika michuano ya Kimataifa.
Waandishi wa habari za Michezo Zanzibar wakifuatilia mkutano huo wa kukabidhi vifaa kwa viongozi wa timu za Mikoa ya Unguja. Makabidhiano hayo, yamefanyika katika ukumbi wa Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar leo.
Kiongozi wa Timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi Ahmada Haji, akitowa shukrani kwa niaba ya timu za Mikoa ya Unguja, baada ya kukabidhiwa Vifaa hivyo na Uongozi wa ZFA Taifa ili kuvitumia katika michuano hiyo vilivyotolewa na Kampuni ya TBL ili kuweza kufanikisha zoezi hilo la kuibua Vipaji kwa Vijana wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment