TANGAZO


Monday, February 17, 2014

Wakuu wa Kampuni ya Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wao wa Afrika watembelea Tanzania

5
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CFAO Motors, Bw. Wayne Mcintosh, akizungumza na Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika katika mpango mkakati wa kubadilishana nao mawazo na uzoefu katika shughuli za biashara na masoko katika ukanda wa Afrika.

Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz ukanda wa Afrika ni kutembelea kampuni hiyo kubwa na ya siku nyingi ya magari hapa duniani na kuangalia aina mpya za bidhaa ambazo zipo sokoni na kupata kujifunza kazi mbalimbali za kijamii ambazo kampuni hiyo ya CFAO Motors inafanya hapa Tanzania.

Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika kutoka nchi za Rwanda, Sudan, Afrika Kusini na nchi zingine wamekuja nchi kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na wamefanikiwa kujifunza shughuli mbalimbali za ufundi na utendaji kazi wa kampuni ya CFAO Tanzania.
6
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika pia walipata fursa ya kuangali akarakana ya kampuni hiyo kwenye maeneo ya Vingunguti na kuona shughuli za ufundi kwa magari yao ambapo wateja ambao wanaharibikiwa na magari wanaweza kupata huduma hiyo kwenye karakana ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.
7
Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard Cambournac akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika.
DSC_0789
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika wakitembelea eneo linalotoa huduma ya kutengeneza kwa teknolojia ya hali ya juu magari ya wateja wa kampuni hiyo pindi yanapopata hitilafu.
DSC_0842
Baadhi ya magari ya wateja wa Kampuni ya CFAO Motors yakisubiri kuhudumiwa.
1
Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors, Wayne Mcintosh (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors, Charles-Edouard CAMBOURNAC, wakati wa Ziara ya kujifunza kutoka Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika. Kushoto ni Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed.
3
Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufika makao makuu ya kampuni hiyo.
8
Baadhi ya kikundi cha wamasai walioburudisha Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika kwa kucheza ngoma za Kimasai.
DSC_0721
Baadhi ya Wakuu wa Mercedes Benz kutoka Ujerumani na Wawakilishi wa Mercedes Benz Afrika wakichukua kumbukumbu za matukio kwenye simu zao wakati kikundi cha Kimasai kilipokuwa kinatoa burudani.
DSC_0708
Meneja Masoko wa CFAO Motors, Bi. Tharaia Ahmed akifurahi jambo na mmoja wajumbe hao.

No comments:

Post a Comment