TANGAZO


Monday, February 17, 2014

Msimu wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 wazinduliwa rasmi

Mmoja wa Waratibu wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014, Fina Mango akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa tuzo hizo, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kaishe, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akizindua Msimu wa Tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014, jijini Dar es Salaam leo.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kaishe, akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akizindua Msimu wa Tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kaishe, wakati alipokuwa akizungumza nao wakati alipokuwa akizindua Msimu wa Tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kaishe, wakati alipokuwa akizungumza nao wakati alipokuwa akizindua Msimu wa Tuzo ya Kilimanjaro Tanzania Music Award 2014, jijini Dar es Salaam leo.
Mmoja wa waratibu wa tuzo hizo, Kurwijira Ng'oko kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), akitoa maelezo kuhusu vipengele vya kushindaniwa katika tuzo hizo, pia kufafanua kuhusu kuondolewa kwa baadhi ya vipengele katika tuzo za mwaka huu. 
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kaishe, akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo tuzo hizo.
Mmoja wa mtoa mada katika uzinduzi huo, akiwasilisha mada kuhusu ushiriki na upendekezaji wa wasanii, kazi na mambo mengine yahusuyo tuzo kijumla.
Baadhi ya waratibu na wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi huo, jijini leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika uzinduzi huo.

Dar es Salaam February 17, 2014. 
KAMPUNI ya Bia ya Tanzania (TBL) kwa ushirikiano na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo tumezindua rasmi msimu mwingine wa Tuzo za Muziki Tanzania zinazojulikana kama KTMA.

Mkutano na wana habari za michezo na burudani kutoka vyombo mbali mbali ndio umezindua msimu huu katika hoteli ya Kebby’s ilioko maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam. Viongozi wa BASATA pamoja na wa bia ya Kilimanjaro walizungumzia mabadiliko chanya katika mchakato wa mwaka huu ikiwa ni juhudi na hatua za kuendelea kuboresha mfumo wa upatikanaji wa wateule wa vipengele mbali mbali vya tuzo hizi.

Mabadiliko:
Mwaka huu watanzania wamepewa fursa ya kupendekeza wasanii, nyimbo, vikundi, watayarishaji, video n.k wanazodhani zinastahili kuwepo kwenye mchakato wa kuwapata wateule wa tuzo za muziki Tanzania. Kwakutumia mfumo wa SMS na mtandao wapenzi wa muziki wataweza kutoa mapendekezo yao kupitia;
a.      Namba ya simu 15440.
b.      Mtandao – Website/tovuti na barua pepe/email.

Semina fupi ilioendeshwa katika hoteli ya Kebbys ilitoa ufafanuzi wa jinsi ya kutoa mapendekezo na wapi mpenzi wa muziki anaweza kwenda kupata maelezo ya ziada yanayohusiana na njia za kutumia kupendekeza kazi na wasanii wanaowataka.

“Baada ya tathmini ya mwaka jana, tumeonelea wakati wa kuwahusisha wapenzi wa muziki umewadia. Tuzo za muziki ni mchakato endelevu unaoendelea kubadilika kila mwaka ikiwa ni jitihada za kuboresha na kuhakikisha mfumo unakua imara, kuhakikisha tunapata wateule na washindi wanaostahili’. Alisema George Kavishe meneja wa bia ya Kilimanjaro.

‘Kama una amini msanii unaempenda ama kikundi ama wimbo n.k inastahili kuingizwa kwenye mchakato, basi pendekeza.’ Alisema George.

BASATA waliwapongeza TBL kwa kuendelea kuwa wabunifu na kuwa makini na tathmini pamoja na taarifa mrejesho (feedback) za wapenzi wa muziki na kuendelea kuzifanyia kazi alimradi kuboresha mfumo mzima wa tuzo hizi za kitaifa.

“BASATA ilipewa nafasi ya kutathmini mchakato huu mpya na tumeuridhia na kuonelea ni mfumo mzuri wenye tija na utakaoleta matoke mazuri zaidi kwa mchakato wa tuzo hizi.” Alisema mwakilishi wa BASATA.

Taarifa kamili za njia ya kupendekeza zipo kwenye mtandao wa Kili http://www.kilitime.co.tz/ktma pamoja na page ya facebook ya Kilimanjaro na kwa taarifa unaweza kuifata handle ya kili @kilimanjarolarger kwenye twitter.

Usiku wa tuzo unatazamiwa kuwa ni tarehe 3-Mei-2014 katika ukumbi wa Mlimani City.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na wasimamizi wa taarifa na mchakato wa KTMA, 1Plus kupitia anuani ilioainishwa hapo chini au na George Kavishe, meneja wa Kilimanjaro.


Kwa taarifa zaidi:

George Kavishe, Brand Manager, Mob: +255 767 266 786, Email: George.kavishe@tz.sabmiller.com. www.kilitimetz.com
1Plus: +255 769 172 535 E: info@oneplus.co.tz au mams20012002@yahoo.co.uk

MWISHO.

 

Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India. SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.


No comments:

Post a Comment