Mkurugenzi wa Angels Moment, Pamela Mathayo (wa pili kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, juu ya Tamasha la Mwanamke na Akiba la kuwaelemisha wanawake kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa mbalimbali, litakalofanyika tarehe 19 hadi 21, Februari mwaka huu kwenye ukumbi wa Dar live, Mbagala jijini. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Teddy Mapunda, Mohammed Ramadhani ambaye ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa Kampuni ya Bakhresa Group Azam (wadhamini wakuu wa tamasha) na Meneja Uhusiano wa Umma wa Angels Moment, Beatrice Milinga.
Mkurugenzi wa Angels Moment, Pamela Mathayo (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, juu ya Tamasha la Mwanamke na Akiba la kuwaelemisha wanawake kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa mbalimbali, litakalofanyika tarehe 19 hadi 21 Februari mwaka huu kwenye ukumbi wa Dar live, Mbagala jijini. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo Teddy Mapunda.
Mkurugenzi wa Angels Moment, Pamela Mathayo (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, kuhusu tamasha hilo, litakalofanyika tarehe 19 hadi 21 Februari mwaka huu, ukumbi wa Dar live, Mbagala jijini. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo Teddy Mapunda.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Angels Moment, Beatrice Milinga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo, kuhusu Tamasha la Mwanamke na Akiba la kuwaelemisha wanawake kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa mbalimbali litakalofanyika tarehe 19 hadi 21 Februari mwaka huu kwenye ukumbi wa Dar live, Mbagala jijini. Kushoto ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa Wadhamini Wakuu Kampuni ya Bakhresa Group-Azam, Mohammed Ramadhani. (Picha zote na Mpigapicha Wetu)
Na Mwandishi
Wetu
KAMPUNI ya
Angels Moment imeandaa Tamasha la Mwanamke na Akiba lenye lengo la kuwaelmisha
wanawake kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa mbalimbali na jinsi ya
kukabiliana na changamoto katika kujiwekea akiba.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Angels Moment,
Pamela Mathayo alisema kuwa litafanyika tarehe 19 hadi 21 Februari mwaka huu
kwenye ukumbi wa Dar live, Mbagala jijini Dar es Salaam.
Alisema
mgeni wa heshima anatarajiwa kuwa Mke wa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa wa Tanzania, mama Asha Bilali na
wataalamu wa masuala ya kibiashara na ujasiriamali watawasilisha mada
mbalimbali
Alisema
tamasha hilo litahusisha maonesho mbalimbali ya bidhaa za akina mama ambapo
wanawake 50 wanatarajiwa kuonesha bidhaa zao na zaidi ya 5000 wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hilo la kwanza na la
kipekee kuwahi kufanyika nchini.
Naye Meneja
Uhusiano wa Umma wa Angels Moment, Beatrice Milinga alisema kuwa ni ya tamasha
hilo ni kuondoa kasumba kuhusu suala la kujiwekea kipato hususani kwa kina
mamam na kujifunza mbinu mbalimbali za kujiomgezea kipato.
Tamasha hilo
limedhaminiwa na Said Salim Bakhressa, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mfuko wa Penshen wa PPF, Mamlaka ya Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA), na Mfuko wa Uwekezaji Tanzania (UTT).
Wadhamini
wengine ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Montage limited, benki ya CRDB,
Ashton Media na Baraza la Biashara la Mikono.
No comments:
Post a Comment