TANGAZO


Wednesday, February 12, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma azindua Kampeni ya Lishe bora wilayani Mpwampwa

Akina mama wa Wilaya mpya ya Mpwapwa wakijipatia elimu ya lishe bora kwa mama na mtoto kwa njia ya vipeperushi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe Mkoa wa Dodoma, uliofanyika kimkoa wilayani humo mwanzoni mwa wiki hii. (Picha zote na John Banda, Dodom)
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akimnywesha uji wa lishe mtoto Devotha Samira, ili kumwongezea virutubisho mwilini wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe bora Mkoa wa Dodoma, uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii, wilayani Mpwapwa. Anayeshuhudia ni mama mzazi wa mtoto Devotha ,Bi. Mariam Samira.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto Anthonia John (kushoto), Elizabeth Rafael (katikati) na Loy Juma, waliopatiwa chakula na dawa kwa ajili ya kuongeza virutubisho mwilini, ikiwa ni moja ya zoezi lililofanywa kwenye uzinduzi wa kampeni ya lishe Mkoa wa Dodoma, mwanzoni mwa wiki hii, wilayani Mpwapwa.

Na John Banda, Dodoma
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi amewaagiza wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya zote mkoani Dodoma kuhakikisha Halmashauri zinatunga mara moja sheria ndogo za
kudhibiti na kukabiliana na wazazi na walezi wasiozingatia kutoa lishe bora kwa watoto wao na akinamama wajawazito.

Dk. Nchimbi ametoa agizo hilo mwanzoni mwa wiki hii, wakati akizindua kampeni ya lishe mkoani Dodoma, iliyofanyika kimkoa wilayani Mpwapwa ambapo pamoja na changamoto nyingine amekiri kuwa hali ya lishe kwenye mkoa wa Dodoma siyo nzuri hasa kwa watoto wadogo na akinamama wajawazito.

Aliongeza kuwa madhara ya ukosefu wa lishe bora mkoani Dodoma yanaonekana wazi akitaja kuwa maradhi na vifo vingi vinaletelezwa na lishe duni, lishe duni vilevile imechangia udumavu wa kimwili na uwezo mdogo kiakili kwa watoto wetu ndio maana hivi sasa kumekuwa na tatizo la kushuka kwa ufaulu katika elimu, kudumaa kwa ubunifu na vipaji katika jamii.

Vilevile Amesma kuwa katika jamii kunapokuwa na ukosefu wa lishe bora kwenye hatua fulani ya makuzi kunatengeneza matatizo ya kiakili na ndio maana leo hii, tunazalisha madereva wasio na uwezo wa kuelewa, kuzishika na kuzingatia sheria za usalama barabarani matokeo yake ajali za kutisha kila kukisha.

Dk. Nchimbi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana kukabili tatizo hili akizitaka mamlaka za serikali za mitaa kulifanya suala la lishe bora kuwa agenda ya kudumu kwenye mikutano yao,
vilevile shule zianzishe vilabu vya elimu ya lishe bora kama ilivyo kwa vilabu vya kupinga Rushwa, vilevile maafisa  lishe wafundishe jamii mbinu za uhifadhi wa mbogamboga na matunda ili vyakula hivi vipatikane msimu mzima wa mwaka.

Kwa upande wake afisa lishe mkoa wa dodoma Bi. Mary Bonaventure amesema kuwa taarifa za wizara ya afya na ustawi wa jamiii zinaonesha kuwa kwa mwaka 2010 mkoa wa ulikuwa na tatizo la udumavu kwa kiwango cha asilimia 56% ukilinganisha na asilimia 42% ya kitaifa. Vilevile  taarifa za timu ya Mkoa ya usimamizi wa afya inaonesha kiwango cha utapiamlo katika mkoa ni asilimia 7.3%. Ukilinganisha.

Taarifa za shirika lisilo la kiserikali la mwanzo bora na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani  WFP zinasema mashirika hayo yataendelea kushirikiana na mkoa na wilaya katika jitihada za kuboresha hali ya chakula na lishe kwa watoto wadogo na akinamama hususani wajawazito)

No comments:

Post a Comment