TANGAZO


Monday, February 10, 2014

Rais Jakaya Kikwete akutana na mjumbe wa EU na Shirika la Global Volunteers la Marekani Ikulu jijini Dar

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea ujumbe wa Umoja wa Ulaya (EU), kutoka kwa Mkurugenzi wa EU, Pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU, kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na  Mkurugenzi wa EU, Pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU, kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Koen Vervaeke (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa EU nchini Tanzania, Balozi  Filiberto Ceriani Sebregondi, bada ya kukutana nao, Ikulu jijini Dar es Salaam leo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (EU), ukiongozwa na Mkurugenzi wa EU, Pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Koen Vervaeke, Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, nchini Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dk. Owdenburg Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo, Februari 10, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jarida toka kwa Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, nchini Marekani. (Picha zote na Ikulu)

No comments:

Post a Comment