Viongozi wakiwa Meza Kuu katika Semina ya Jukwaa la Katiba, iliyotayarishwa na Taasisi ya Utafiti na Sera, mjini Zanzibar leo.
Baadhi ya washiriki wa semina ya kuchangia Mjadala wa Katiba uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) na kuwashirikisha wananchi mbalimbali, wanasiasa na viongozi wa Dini Zanzibar, kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba. (Picha zote na Habari kwa hisani ya Zanzi News Blog)
WAKATI mkutano maalum wa bunge la katiba ukitarajiwa kuanza Februari 18, wajumbe kutoka Zanzibar wametakiwa kuweka mbele maslahi ya nchi badala ya vyama.
Aidha wameonywa kwamba kama fursa hiyo wataichezea watajuta maishani mwao pamoja na kusababisha mashaka makubwa makubwa kwa vizazi vyao.
Wakichangia mjadala wa katiba uliofanyika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kampasi ya Vuga, washiriki, walitahadharisha kwamba kama Zanzibar itazembea na kuweka mbele maslahi ya vyama, matatizo yaliyopo sasa yatakuwa makubwa zaidi siku za usoni na wakati huo hakutakuwa na mtu wa kuyasema kwa sababu fursa ilitolewa ikachezewa.
Akifungua mjadala huo, Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, Mshibe Ali Bakar, aliwatoa hofu wajumbe akisema wasihofu kuzungumza kwa sababu tu miongoni mwa wajumbe wamo viongozi wa serikali na vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment