TANGAZO


Monday, February 10, 2014

Maalim Seif awahutubia wananchi na Wana-Cuf Chake Pemba

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Maliim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba, katika mkutano wa hadhara wa chama hicho, uliofanyika katika kiwanja cha Tibirinzi Chake Chake.
Wajumbe wa Kamati ya maridhiano Zanzibar, wakibadilishana mawazo, huko katika kiwanja cha Tibirinzi Chake Chake Pemba, katika mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF). Kutoka kulia ni Ndg. Edi Riyam, Ndg. Mansour Yussuf Himid, Mhe. Ismail Jussa, Mhe. Aboubakar Khamis Bakari na Mzee Hassan Nassor Moyo.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa katika mkutano huo, kisiwani Pemba jana.
Akinamama wa kikundi Cha ngoma ya msewe kutoka kambini kichokochwe, wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma hiyo ya asili kisiwani Pemba, huko katika kiwanja cha Tibirinzi chake Chake katika mkutano wa hadhara wa CUF. (Picha na Abdi Suleiman wa Zanzi News, Pemba.)

No comments:

Post a Comment