TANGAZO


Saturday, February 22, 2014

Pande pinzani zalaumiwa Sudan Kusini





Mzozo wa Sudan kusini


Ripoti ya mda ya Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Sudan Kusini inasema kuwa vikosi vya serikali na vile vya waasi vilikiuka haki za kibinaadamu huku raia wa kawaida wakibeba mzigo huo.
Imesema kuwa maafa yaliotekelezwa, ikiwemo ubakaji, mauaji ya halaiki na mateso yalitekelezwa kikabila.
Umoja wa mataifa ulinukuu ripoti kwamba wanajeshi wa serikali walio watiifu kwa rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka waliwaua watu wa kabila la Nuer katika mji mkuu wa Juba katika siku za kwanza za mzozo huo.
Aidha Umoja wa Mataifa ulipata ushahidi kwamba vijana waliojihami wa kabila la Nuer waliwaua raia wa kabila la Dinka katika mji wa Malakal.
Ripoti hiyo iliangazia siku saba za kwanza za mzozo huo uliozuka katikati ya mwezi Disemba.

No comments:

Post a Comment