TANGAZO


Saturday, February 22, 2014

Uchina yapinga mkutano wa Dalai Lama


Dalai Lama na rais Obama wa Marekani


Uchina imemuagiza balozi wa marekani nchini humo kufika mbele yake kama hatua ya kupinga mazungumzo kati ya rais Obama na kiongozi wa kidini wa eneo la Tibet aliye mafichoni Dalai Lama.
Naibu waziri wa maswala ya kigeni nchini Uchina Zhang Yesui amemwambia mjumbe huyo wa marekani kwamba serikali ya marekani italazimika kufanya kila juhudi kuimarisha uhusiano wake na Uchina.
Wakati wa mkutano wake na Dalai Lama,rais Obama amesisitiza umuhimu wa kuunga mkono na kuzilinda haki za binaadamu wa eneo la Tibet.
Mkutano huo mjini Washington uliendelea licha ya onyo kutoka Uchina kwamba utaharibu uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.
Ikulu ya whitehouse imesema kuwa Dalai Lama alipokelewa kama kiongozi wa dini na tamaduni anayeheshimiwa kimataifa na wala sio kama kiongozi wa taifa.

No comments:

Post a Comment