Kulingana na mkataba huo uliosimamiwa na mawaziri wa maswala ya kigeni kutoka umoja wa bara ulaya,serikali ya mpito itabuniwa na Uchaguzi kufanywa mwezi wa Disemba.
Aidha makubaliano hayo yanarejesha sheria ya kumpunguzia mamlaka rais,swala ambalo tayari limepitishwa na bunge.
Aidha bunge lilipitisha sheria ambayo itamuachilia huru kongozi wa Upinzani Yulia Tymoshenko.
Wakati huohuo makumi ya maelfu ya waandamanaji bado wamesalia katika medani ya uhuru katikati ya mji mkuu wa Kiev usiku kucha.
Waandishi wanasema kuwa waandamanaji hao wana hofu kwamba huenda mkataba huo usitekelezwe.
Waandamanaji hao waliwazoma viongozi wa upinzani waliposimama katika jukwaa ili kuwahutubia baada ya kutia sahihi mkataba huo.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kundi moja la waandamanaji limetishia kuvamia majengo ya bunge iwapo rais Yanukovych hatajiuzulu kufikia leo asubuhi.
Awali kulikuwa na matukio ya kusikitisha baada ya majeneza ya watu 77 waliouawa wakati wa siku tatu za ghasia hizo kuwasilishwa katika medani ya uhuru.
No comments:
Post a Comment