Naibu Waziri wa Fedha
Adam Malima (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa, mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya Mkoa wa Mara jana.
Naibu Waziri wa Fedha
Adam Malima akiongea na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara juu ya umuhimu wa
utumiaji wa mashine za kodi za kielektroniki (EFDs) kwa wafanyabiashara hao
kukusanya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ili Serikali iweze kutoa mahitaji
ya kijamii na uchumi kwa wakati.
Kamishna wa Kodi za
Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Patrick Kasera akifafanua jambo kwa
wafanyabiashara wa mkoani Mara juu ya mashine za EFDs na kusema kuwa mashine
hizo kazi yake kuu ni kutunza kumbukumbu za biashara hasa manunuzi na uuzaji na
sio mfumo wa kodi kama ilivyopokelewa mwanzoni na wafanyabiashara nchini.
Baadhi ya
wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima (hayupo
pichani) alipokuwa alipozungumza na wafanyabiashara hao jana, mjini Musoma katika
ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo.
Baadhi wa wajumbe
waliohudhuria kikao cha wafanyabiashara wa mkoa wa Mara wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima alipozungumza nao ili kuwaelimisha juu ya masuala
mbalimbali ikiwemo mashine za EFD wakati wa ziara yake ya kikazi mikoa ya kanda
ya Ziwa.
Baadhi ya
wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima alipokuwa
alipozungumza na wafanyabiashara hao jana mjini Musoma katika ukumbi wa Ofisi
ya Mkuu wa mkoa huo wakati wa ziara yake ya kikazi mikoa ya kanda ya Ziwa. (Picha zote na Mpigapicha wetu)
No comments:
Post a Comment