TANGAZO


Sunday, February 2, 2014

Maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yafana jijini Mbeya

*JK amsifu Kinana na timu yake kwa kuchapa kazi
 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwapungia wananchi, alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho, Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya leo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana. JK alimpongeza Kinana kwa kuonesha  njia na kutoa mfano kuhusu kufanya kazi ya chama ndani ya umma.
 
"Katika ziara zake mikoani akifuatana na baadhi ya Makatibu wa Sekretarieti na viongozi wengine wa CCM, amekuwa  anafanya kazikubwa na nzuri sana. Na kwamba ziara zake zinakijenga chama na kutoa tawsira nzuri ya chama katika jamii", alisema JK. Pia alisema ziara za Kinana zinahuisha uhai wa chama hicho.

Rais Kikwete aliendela kusema kuwa Kinana amekuwa akifanya  mambo  ambayo hayajazoeleka kufanywa. "Ametembelea maeneo ambayo si viongozi wengi hufika. Wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha wengi", aliongeza 
 
"Hukaka na wananchi, anakula nao na kufanya nao kazi. Na kubwa zaidi amekuwa anatoa fursa kwa wananchi kuelezea matatizo yanayowasibu, manung'uniko yao na kero zao pia", alimaliza JK. (Picha zote na Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio Blog)
 Kinana akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho, ambapo alisisitiza kuendeleza utaratibu alionao wa chama hicho kuwa karibu na wananchi, pamoja na kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
JK akionesha mfano wa Jembe na Nyundo alama za chama hicho zinazomaanisha kwamba nchi inaongozwa na wafanyakazi na wakulima.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii maarufu nchini, baada ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama hicho, wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwapiga picha wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers) waliokuwa wakipiga picha ya paoja na Rasi Kikwete baada ya maadhimisho kumalizika.
Wafuasi wa CCM waliotimiza miaka 37, wakirusha njiwa 37 ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Msanii Ummy Wenslaus (Dokii), akionesha vimbwanga vyake alipokuwa akitumbuiza kwa wimbo wake wa CCM wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Rungwe, Richard Kasesera (kulia), wakicheza ngoma ya ling'oma wakati wa maadhimisho hayo.
Kundi la TOT likiongozwa na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa likifanya mambo wakati wa maadhimisho hayo.
Wasanii wa muziki na filamu wakiwapungia mikono wananchi baada ya kujiunga na CCM leo.
Sehemu ya umati wa wananchi ukiwa katika sherehe za maadhimisho hayo.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi nyaraka za Bajaj, mlemavu wa mikono ambayo alimwahidi akiawa ziarani Mbeya siku zilizopita
JK akitimiza ahadi yake kwa kumkabidhi Bajaji mlaemavu wa miguu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akipiga gita alilolinunua kwa ajili ya kumpatia msaada msanii Petro Abel 'Awilo' (kulia), wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya leo. Katikati anayepiga makofi ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
JK akikabidhi gitaa hilo, iiwa ni kutimiza ahadi aliyomwahidi msanii huyo mwaka jana.
 Msanii huyo akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa gitaa hilo.
JK na Kinana wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa vyuo vikuu waliojiunga na chama hicho.

No comments:

Post a Comment