TANGAZO


Sunday, February 2, 2014

Matembezi ya mshikamano kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa CCM jijini Mbeya

 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi wakati wa matembezi ya mshikamano, kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho, yaliyoanzia Soweto hadi Bustani ya Jiji la Mbeya leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kulia ni Makamu Mwenyekiti, Philip Mangula. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akiwa na watoto wakati wa matembezi ya kuadhimisha miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya leo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana (katikati kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya (katikati), wakiwa pamoja na baadhi ya wanachama na wananchi, wakitembea wakati wa matembezi ya kuadhimisha miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya leo. Matembezi hayo yalianzia Soweto hadi Bustani za jiji hilo.
Mwananchi akiwa ameshika nyundo na jembe alama muhimu ya Bendera ya CCM, ambazo zinamaanisha mkulima na mfanyakazi.
 JK akiongoza matembezi hayo leo jijini Mbeya
 Baadhi ya wandishi wa habari, wakiwa kazini wakati wa matembezi hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akiwa pamoja na watoto na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula (kulia), wakiwa kwenye matembezi hayo.
Mfanyabiashara wa nguo za mitumba (machinga), akiwa amejumuika na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wengine kwenye matembezi hayo ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho leo.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mbeya wakiungana kwenye matembezi hayo na wanachama wa CCM,  eneo la Uwanja wa Sokoine leo.

No comments:

Post a Comment