KATIKA siku za hivi
karibuni kumeibuka kundi la baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na wanasiasa ambao
wanapita sehemu mbalimbali nchini kupotosha umma wa Watanzania kuhusu zoezi la
kujadili rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania. Viongozi hao wamefikia hatua
hatakuwachanganya wananchi kuhusu nini ikinachotakiwa kufanywa katika mchakato
unaoendelea wa kujadili rasimu ya Katiba Mpya. Wengine wanaielezea rasimu ya
Katiba Mpya kama katiba kamili iliyopitishwa kutumika sasa.
Serikali inapenda
kutoa ufafanuzi kwamba mjadala kuhusu Katiba mpya haujafungwa na wananchi
wanapaswa kuendelea kujadili na kutoa maoni yao kwa uwazi bila kuingiliwa ama
kulazimishwa na mtu yeyote.
Ieleweke pia kwamba
kilichopo hivi sasa ni rasimu ya Katiba, siyo Katiba Mpya. Mchakato wa kupata
Katiba Mpya ndio kwanza umeingia katika hatua ya kwenda kujadiliwa katika Bunge
Maalum la Katiba ambalo litaamua nini maudhui ya Rasimu ya Katiba Mpya kabla ya
kupelekwa kwa wananchi kupigiwa kura.
Ndugu
wananchi ni vema ikafahamika kuwa Bunge
Maalum la Katiba ndilo lenye mamlaka ya mwisho ya kubadilisha , kurekebisha ,
kufuta ama hata kuingiza vipengele vipya vya rasimu ya Katiba.
Ni
vema wananasiasa mkaacha kutumia Rasimu hiyo kuwapotosha wananchi kuwa na
kuwafanya wafikiri kuwa tayari kuna
Katiba mpya .
Imetolewa
na Idara ya Habari (MAELEZO)
No comments:
Post a Comment