TANGAZO


Wednesday, February 19, 2014

Mama Asha Bilal alifungua Tamasha la Mwanamke na Akiba, Mbagala jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi  Mkuu wa Angles Moments Naima Malima, akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mke wa Makamo wa Rais, Asha Bilali katika ufunguzi wa tamasha la Mwanamke weka Akiba litakalofanyika kwa siku tatu.
Mkurugenzi  Mkuu wa Angles Moments Naima Malima, akisoma risala ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mke wa Makamo wa Rais, Asha Bilali katika ufunguzi wa  tamasha la Mwanamke weka Akiba litakalofanyika kwa siku tatu.
Mke wa makamo wa Rais Asha Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Mwanamke weka Akiba, akisoma risala ya ufungunzi wa tamasha hilo, leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Dar live Mbagala.
Mke wa Makamo wa Rais Asha Bilali na mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda wakiangalia tunzo aliyokabidhiwa  katika Tamasha la Mwanamke weka akiba, leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Dar live Mbagala.
Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Esther Sumaye akiwasalimia wajumbe waliofika katika ufumbuzi wa Tamasha la Mwanamke weka akiba. Anayepiga makofi mbele ni Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Regina Lowassa na Mke wa Makamo wa Rais, Mama Asha Bilali.
Meneja Uhusiano  na Masoko wa  Mfuko wa Pesheni PPF, Lulu Mengele (kulia), akipokea tuzo ya udhamini kutoka kwa Mke wa Makamo wa Rais, Mama Asha Bilali katika Tamasha la Mwanamke weka Akiba, leo jijini Dar es Salaam.
Mke wa Makamo wa Rais, Mama Asha Bilali ambaye alikuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Mwanamke weka Akiba, akikata utepe ikiwa ishara ya kufungua rasmi tamasha hilo, leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Dar live Mbagala.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia asali kwa Mgeni rasmi, Mke wa Makamo wa Rais, Mama Asha bilali katika Tamasha la Mwanamke weka Akiba, leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa tamasha la Mwanamke weka akiba wakifuatilia kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika viwanja vya Dar live Mbaggala. (Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)

No comments:

Post a Comment