TANGAZO


Thursday, February 13, 2014

Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Azungumza na Balozi wa Israel Nchini Tanzania

Balozi Seif akisalimiana na Balozi wa Israel nchini Tanzania, Gil Haskel, wakati wakijiandaa na mazungumzo ya kuimarisha uhusiano kati ya Israel na Zanzibar, jijini Dar es Salaam leo.
Balozi wa Israel nchini Tanzania, Gil Haskel akimpongeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, kufuatia Tanzania kuendeleza mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika misingi ya amani na utulivu. (Picha zote na Hassan Issa wa – OMPR)


Na Othman Khamis Ame, OMPR.
SERIKALI ya Israel imekusudia kuunga mkono harakati  za Kiuchumi na Maendeleo ya Zanzibar ili kuona ustawi wa  maisha ya Wananchi wa Zanzibar  katika dhana nzima ya kukabiliana na ukali wa maisha na kupunguza umaskini inafanikiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi wa Israel nchini Tanzania Bwana Gil Haskeli aliyefika nyumbani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Bara bara ya Haile Selassie jijini Dar es Salaam leo kwa mazungumzo ya kuimarisha uhusiano kati ya pande hizo mbili.

Balozi Gil Haskel alisema amemua kufanya ziara maalum ya kutembelea na kukutana na Viongozi wa juu na waandamizi wa Wizara zinazohusika na Sekta za Kilimo na  Afya Zanzibar ili kuangalia mazingira ya namna ya kuanza kutekeleza mpango huo.

Alisema Israel tayari imeshajitolea kusaidia mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Wizara za Afya na Kilimo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kitaaluma utakaowapa fursa na nguvu kubwa ya kutekeleza majukumu yao Kitaalamu zaidi.

“ Tumeamua uwezo wetu wa Kitaaluma katika sekta za Kilimo na Afya tulionao katika kipindi kirefu hasa suala la kilimo cha umwagiliaji { Drop Irrigation } tunaweza kuwasaidia wenzetu ili nao wapige hatua za maendeleo “. Alisema Balozi Gil Haskel.

Balozi Gil ameipongeza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kutokana na hatua yake ya kuendelea na mchakato wa kuelekea kwenye Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment