TANGAZO


Sunday, February 16, 2014

Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), mjini Dodoma

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Rais  Jakaya Kikwete akiashiria jambo kabla ya kuanza kwa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Taifa (NEC), ukumbi wa White House mjini Dodoma leo. Kushoto ni Makamu wake, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana. (Picha zote na Ramadhan Othman)
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC), wakisimama kuimba wimbo wa chama chao, wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais  Jakaya Kikwete, alipoingia ukumbi kuendesha mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM (NEC), wakiangalia magazeti kupata habari  mbalimbali kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), wakisikiliza taarifa na mada zilizokuwa zikiendelea katika kikao hicho, mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment