TANGAZO


Wednesday, February 19, 2014

Kikao cha Bunge maalum la Katiba mpya Mjini Dodoma leo

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba nje ya ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwanasiasa mkongwe na Kanda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge, kabla kuingia kwenye ukumbi wa bunge hilo maalum leo.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kutoka Visiwani Zanzibar, wakijadili jambo nje ya ukumbi wa Bunge hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Chritopher Mtikila kulia akijadili jambo kuhusu Tanganyika na Muungano na baadhi ya wajumbe wa Bunge maalum kutoka Tanzania Bara.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, akizuwaeleza jambo Wabunge wa Kigoma Zitto Kabwe (kulia) na Albert Obama.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akizungumza wakati akiendesha kikao cha Bunge hilo. 
Baadhi wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakipitia Rasimu za Kanuni za Bunge Maalum.
Mjumbe kutoka Zanzibar, Mohamed Aboud akizungumza na wajumbe kutoka kushoto, Profesa Lipumba, Hussein Mwinyi na Profesa Mark Mwandosya, wakati wa kikao hicho mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakigawiwa Rasimu za Kanuni za Bunge Maalum.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, akizungumza na wajumbe, wakati akiendesha kikao cha Bunge hilo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kuaghirishwa leo mpaka kesho.

No comments:

Post a Comment