TANGAZO


Wednesday, February 19, 2014

NMB yadhamini Mkutano Mkuu wa Makamanda wa Jeshi la Polisi

Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro

BENKI ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 75, kudhamini mkutano mkuu wa siku sita wa Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini unaoendelea katika chuo cha taaluma ya Jeshi la Moshi (MPA), Mkoani Kilimanjaro.

Mkutano huo ambao unajumuisha makamishna, makamanda wa mikoa ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao makuu, ulizinduliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe.Pereira Sirima. 
Naibu waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Ame Sirima akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), kwenye mkutano mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, mkutano huo umedhaminiwa na NMB.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya NMB, wakifurahi walipokuwa wakijadili jambo, wakati wa uzinduzi wa mkutano wa Maofisa wa Jeshi la Polisi.
Naibu waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Sirima (katikati), IGP Ernest Mangu (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, wakiwa katika uzinduzi wa mkutano wa Maofisa wa Jeshi la Polisi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima akihutubia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima, akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Jeshi la Polisi wakiwemo wadhamini wa mkutano huo benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment