Shirika la misaada la Medecins Sans Frontiers, linasema kuwa ghasia katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, zimekithiri na kufika viwango vya kutisha sana kiasi cha kutia wasiwasi na kwamba msaada unahitaji kupelekwa nchini humo haraka iwezekanavyo.
Shirika hilo limetuhumu jamii ya kimataifa kwa kutelekeza watu wa nchi hiyo na kutoa wito kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na mataifa ya Afrika kuchukua hatua za dharura kukomesha ghasia na maafa huko.
Rais wa shirika hilo, Dr Joanne Liu, aliambia BBC kuwa raia wengi wanahofia usalama wao na kuwa wanahofia kutafuta hifadhi hospitalini ikiwa hawatapata ulinzi wa shirika la MSF.
No comments:
Post a Comment